MHE. RAIS DKT. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI SULUHU SPORTS ACADEMY MKUNGUNI-KIZMKAZI ZANZIBAR

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt, Samia Suluhu Hassan leo August 22,2024 ameweka Jiwe la Msingi la mradi wa Ujenzi wa Suluhu Sports Academy iliyojengwa na wadau wa Maendeleo wakiongozwa na CRDB Foundation ambapo ndani yake kutakuwa Viwanja vya Michezo mbalimbali ikiwemo Uwanja wa mpira wa miguu wenye uwezo wa kuchukuwa Watazamaji 20,000.

Awamu ya kwanza ya Ujenzi wa academy hiyo inatarajiwa kukamilika Mwezi April mwakani.

Uwekaji wa Jiwe la Msingi ni sehemu ya Shamrashamra za Tamasha la Kizimkazi festival 2024.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000