KAMATI YA LAAC YAWAHOJI KONDOA DC UJIBUJI WA HOJA ZA CAG

Kamati ya Bunge ya LAAC imehoji Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa kuhusu hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) alizozotoa wakati wa ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa hospitali wa Wilaya hiyo.

 Kamati imehoji hayo wakati wa ziara ya Kamati hiyo wilayani humo iliyofanyika tarehe 15.03.2024.

Hoja zilizohojiwa na Kamati kuhusiana na ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Kondoa ni pamoja vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 3.6 kutoomekana stoo, PVC, sakafu katika jengo la uzazi kuvimba na kubanduka, nyufa kwenye ukuta na nyongeza ya Sh milioni 260 ya kukamilisha mradi huku watendaji wa halmashauri hiyo kupata ugumu wa kujibu hoja.

Mwenyekiti wa LAAC, Mhe. Halima Mdee alihoji uongozi wa halmashauri kushindwa kumwonyesha CAG udhibitisho wa mahitaji fedha hizo Sh milioni 250 zilizotajwa kwa ili kukamilisha mradi huo.

 “Tupatieni uhalali wa nyongeza mnayoitaka katika kukamilisha mradi huu. Sisi nia yetu ni kuona jamii inawajibika katika kutunza na kulinda fedha za nchi hii,” alisema.

Neye, Mjumbe wa Kamati wa hiyo Mhe. Esther Bulaya amehoji nini kimesababisha hoja za CAG ikiwemo kutouonekana kwa vifaa vyenye thamani ya Sh milioni 3.6, sakafu kubanduka, PVC kubanduka na nyufa.

Akifafanua kuhusu hoja hizo Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-TAMISEMI (anayeshughulikia elimu) Dk Charles Msonde amesema uadilifu mdogo na usimamizi usio makini umekuwa ukikwamisha utekelezaji wa miradi katika serikali za mitaa.

 Alisema msingi mzima wa miradi ya Serikali ya Mitaa kutokamilika katika maeneo mengi ni kukosekana kwa uadilifu mdogo na usimamizi usio makini.

Awali, Ofisa Mipango wa Halmashauri hiyo, Joshua Mnyangale alisema Sh bilioni 1.8 zilitengwa kwa ajili ya ujenzi wa hospitali hiyo ulioanza Juni 20, 2020 na zilipokelewa kwa awamu tatu.

Alisema kulikuwa na changamoto kadhaa katika kutekeleza mradi huo ikiwemo ya muinuko mkubwa wa eneo la ujenzi kwenye jengo la mama na mtoto, kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi na kutofautiana kwa gharama ya vifaa vya ujenzi ukilinganisha na uhalisia katika utekelezaji wa mradi.

 Mbunge wa Kondoa Mjini, Alli Makoa alisema kuwa kutokuwa na nyaraka za uthibitisho wa nyongeza hiyo kunatia mashaka na kuonesha halmashauri inatumia vibaya fedha za miradi au hawana uwezo wa kuandika ripoti hizo za miradi.

 Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Dk Mkanachi alisema alichokiona katika mradi wa shule ni kukosekana kwa usimamizi mzuri na uwezo mdogo na wataalamu kutoweka kumbukumbu za miradi jambo ambalo imekuwa ikishindikana kupatikana kwa takwimu sahihi za miradi.

 Naye Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Shabani Millao aliahidi kwenda kuyafanyia kazi maelekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo, naamini kuwa siku zijazo hayatatokea tena.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000