DKT SAMIA “SERIKALI IMEVUNA BILIONI 60.2 ZA SGR NA KIZALISHA AJIRA ZAIDI YA 900.
Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambae pia anatetea nafasi yake kwa muhula wa pili ameweka wazi mafanikio waliyoyapata kama serikali kupitia mradi mkubwa wa reli ya kisiasa ya umeme (SGR) kuwa ni Bilioni 60.2 na kutoa ajira zaidi ya 900 kwa Watanzania huku ujenzi huo ukiendelea kwa maeneo mengine.
” Kwa upande sekta ya uchukuzi nikianza na reli ya SGR, Utekelezaji wa mradi wa relj ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro imekamilika kwa asilimia 100 huku ujenzi SGR kuingia bandarini umefika asilimia 91.78″.
“Tunataka kuingiza SGR bandarini ili kurahisisha usafirishaji wa mizigo kutoka bandarini kwenda yanapokwenda”.
Rais Dkt. Samia ameyasema hayo katika ufunguzi wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi (CCM) viwanja vya Tanganyika Packers vilivyopo Kawe, Kinondoni Dar es Salaam, kuelekea uchaguzi Mkuu wa Rais Wabunge na Wadiwani Octoba 29, 2025.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000