Yanga hakuko shwari
Taarifa zilizotufikia hivi punde kutoka ndani ya kikao cha uongozi wa Yanga ni kwamba Rais wa Yanga Injinia Hersi amesusa na kutoka kwenye kikao baada ya mjumbe mmoja wa kikao hicho kumtuhumu kuwa anadanganya na hasemi ukweli kwenye mambo mengi ,kitu kinachopelekea wachezaji wengi hasa wa Congo kutaka kuondoka klabuni hapo.
Huku sakata hilo likiendelea chanzo chetu kinatujulisha kuwa makamu wa Rais wa Yanga bwana Arafat anafanya juhudi za kupigia viongozi wa serikali kunusuru hali hiyo ya sintofahamu iliyotokea ndani ya kikao hicho.
Kwa taarifa hizi ni wazi sasa bundi ametua rasmi kwenye klabu ya Yanga ambapo kuna sintofahamu kubwa baada ya kocha Nabi kuondoka pasipo kutegemewa wiki iliyopita.
Tutaendelea kuwapa habari hizi za ndani ndani sana kadri zinavyotufikia hasa kwenye hii sehemu ya makamu kuwapigia simu viongozi wa serikali. Tunajiuliza kwani Yanga ni timu ya serikali au ni timu ya taifa?
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000