WAZIRI MKUU MHE.MAJALIWA AZINDUA JENGO LA UTAWALA LA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG’HWALE – GEITA
Na mwandishi wetu
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa leo tarehe 02.06. 2024 ameweka jiwe la msingi la jengo la utawala la halmashauri ya wilaya ya Nyangh’hwale ambalo ujenzi wake umefikia 85% za ujenzi wake.
Akizungumza baada ya uwekaji wa jiwe la msingi la jengo hilo ambapo mpaka sasa limegharimu shilingi za kitanzania zipatazo bilioni 3.7.
Waziri Mkuu Mhe. amesema kuwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kutoa fedha kwa ajili ya kuimarisha majengo ya utawala kwenye halmashauri zetu “Lengo la Rais Dkt. Samia ni kuona wananchi wanapata huduma karibu na maeneo yao”.
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amewataka wakuu wa idara na watumishi wengine kwenye halmashauri kuendelea kufanya kazi kwa bidii, weledi na uadilifu mkubwa katika kuwahudumia wananchi “Wananchi wana matumaini makubwa na Serikali yao, wahudumieni na mtatue kero zao”
#KigogoMediaUpdates
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000