WANAFUNZI WENYE UFAULU KATI YA 121 – 300 WOTE WAMEPANGIWA SHULE
Published on: 4 days ago
Dodoma
Uchaguzi wa Wanafunzi wa Kujiunga na Kidato cha Kwanza mwaka, 2025 umezingatia kigezo cha ufaulu wa mtahiniwa anayechaguliwa. Kila mtahiniwa aliyefanya Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi mwaka, 2024 na kupata jumla ya alama za ufaulu kati ya 121 hadi 300 amechaguliwa na kupangiwa Shule ya Sekondari ya Serikali.
Uchaguzi huu umehusisha wanafunzi 974,332 sawa na asilimia 100 ya wanafunzi wote waliokuwa na sifa ya kuchaguliwa wakiwemo Wasichana 525,225 na Wavulana 449,107. Wanafunzi hao ni wale waliofanya na kufaulu Mtihani wa Kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka, 2024.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000