Wakili Nshala anatapatapa au kachanganyikiwa

Ni kichekesho sana kwa mtu kama Nshala kutoa tuhuma za kijinga na za kuchekesha kuwa anataka kuuwawa. Nshala alivamia mambo asiyoyajua kisa tu mama yake mlezi Profesa Tibaijuka katumwa kutopoka na Karamagi kuhusu bandari basi naye akaingia kwenye mkumbo.

Yaani Nshala una athari gani mpaka utishiwe kuuwawa? Yaani wewe Nshala nani akuuwe na kwa sababu gani? Huna madhara na hujawahi kuwa na madhara. Wewe ni miongoni mwa watu waoga sana ambao wakati wa Magufuli mlifyata mkia kama hakuna kilichokuwa kinaendelea. Wakati Karamagi anaingia mkataba wa kihuni na wa hivyo ulikuwa wapi? Au ilikuwa sawa kipindi kile?

Kwani GSM aliyewapa hela mkafungue kesi mahakama kuu kupinga uwekezaji bandarini anashindwaje kukulinda kama kweli unataka kuuwawa? Wewe ni mwanasheria na unajua vitisho vya aina hii vinaripotiwa polisi, kuja kuanza kuleta hoja za kitoto hivi ni dalili za kuwa unatapatapa sana na kufanya ujinga wako uonekane wazi wazi sana.

Hakuna atakayekuuwa na hakuna anayekutisha wewe bwana Nshala unajitisha mwenyewe na unatengeneza matukio tu ya kupata huruma kwa wafadhili wenu wa yale makesi yenu ya katiba huko mahakama yenu ile ya Arusha

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000