UZINDUZI WA NDEGE MPYA YA BOEING 787-8 DREAMLINER WAONGOZWA NA RAIS WA ZANZIBAR DKT HUSSEIN ALI MWINYI.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amewaongoza Viongozi na Wananchi mbalimbali katika mapokezi ya ndege mpya ya Boeing 787 -8Dreamliner iliowasili nchini  tarehe 20 Agosti 2024 katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.

Ndege hiyo iliotoka moja kwa moja nchini Marekani ilikotengenezwa kwa shillingi za kitanzania Billioni 300 inakuwa ndege ya 16 kununuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk, Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kuwekeza katika sekta ya anga kwani njia muhimu ya kufungua milango ya kiuchumi na kuunganisha nchi na mataifa mengine kimaendeleo.

Rais Dk, Mwinyi amefahamisha kuwa ndege hiyo mpya imenunuliwa kwa bajeti ya ndani ya Serikali na kuwashirikisha baadhi ya washirika wa Maendeleo.

Aidha amesisitiza kuwa ni utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2025 na kukamilisha mpango mkakati maalum wa kuliimarisha shirika la ndege la Tanzania ATCL.

Amesisitiza kuwa kuwepo huduma za Anga za uhakika kutaongeza idadi ya Watalii wanaokuja nchini kutaka bodi ya shirika la ndege la ATCL kusimamia viwango vya Bora katika utoaji wa huduma kuwavutia abiria wa ndani na nje ya nchi.

Rais Dk, Mwinyi ametoa rai kwa Mamlaka ya anga Tanzania kuhakikisha kuwa na safari nyingi zaidi katika maeneo yenye vivutio vya utalii ili kuinua sekta hiyo kupita usafiri wa anga .

Rais Dk, Mwinyi ameishauri ATCL kuongeza safari nyingi za kimataifa kupitia Zanzibar kwa dhamira kukuza utalii Pamoja na khkifungua kisiwa cha Pemba kiutalii kwa kuna vivutio lukuki ambavyo vinahitaji kutangazwa.

Amempongeza kuwa sekta ya utalii ni muhimu kwani inachangia asilimia 30 ya ukuaji wa Uchumi wa Zanzibar hivyo kuwa huduma Bora za ndege ni jambo la lazima.

Amezipongeza juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, Samia Suluhu Hassan za kuendeleza kullimarisha shirika la ndege la Tanzania kwani limeijengea heshima kubwa nchi na kuwa miongoni mwa maßhirika yenye ndege nyingi kwa nchi za Kusini mwa Afrika.

Amesisitiza Mamlaka ya Usafiri wa Anga kusimamia ipasavyo sera na sheria za Usafiri wa Anga ili Mashirika zaidi ya kimataifa kutumia Viwanja vya ndege ziliopo nchini pamoja na kumaliza changamoto ziinazojitokeza katika utoaji wa huduma katika usafiri wa anga.

Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Dk, Khalid Salum amesema kuna faida kubwa kwa nchi kuendelea kuwekeza katika shirika la ndege la ATCL.

Waziri wa Uchukuzi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, Makame Mnyaa Mbarawa amefahmisha kuwa kuja kwa ndege hiyo ni muendelezo wa kukamilika kwa mpango mkakati wa kufungua ATCL ulionza mwaka 2016.

Amesema Serikali itaendelea kununua ndege zaidi kufanikisha mpango huo sambamba na kuliimarisha Viwanja vya ndege katika mikoa mbali mbali hapa nchini

Ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner imewasili majira ya saa moja usiku na hatimae Rais wa Zanzibar Mh Dk, Hussein Ali Mwinyi ameizindua rasmi na kuifanya ATCL kuwa na ndege 16 hadi sasa.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000