UMMY AENDELEA KUWANADI WAGOMBEA WENYEVITI WA MITAA KATIKA KATA NNE ZA TANGA MJINI

Tanga Mjini

Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Mhe Ummy Mwalimu tarehe 22/11/2024 amehudhuria mikutano ya kampeni za wagombea nafasi ya uenyekiti wa Mitaa katika kata 4 za Jimbo la Tanga Mjini ambazo ni Kata ya Maweni  (Mtaa wa Kasera), Kata ya Chumbageni (mtaa wa Chumvini), Kata ya Nguvumali (mtaa wa Gofu Juu C) na Kata ya Mzingani (mtaa wa Suji).

Mhe Ummy amewaomba na kuwasisitiza wananchi wa kata hizo kuwachagua wagombea waliosimamishwa na CCM ili wakashirikiane na viongozi wa CCM  kuwaletea maendeleo katika mitaa yao na kuongeza kuwa viongozi wa mitaa ndio viongozi wa kwanza kabisa kukutana na changamoto za wananchi hivyo wanapaswa kuchagua viongozi sahihi wanaotokana na CCM

Aidha Mhe.Ummy ameendelea kumshukuru Mhe Rais Dr Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuleta fedha nyingi za miradi ya maendeleo katika jiji la Tanga na hivyo CCM Tanga Mjini kupata nguvu ya kuwaombea kura wagombea wa mitaa wanaotokana na CCM.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000