TUNATAKA MAENDELEO KWA AJILI YA WATU WETU – DKT. BITEKO

Namonge

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)Taifa ambaye pia ni Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amesema katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa mwaka 2024, CCM imedhamiria kuendelea kutekeleza miradi  ya maendeleo ili kubadilisha hali za maisha ya wananchi.

Amesema Kata ya Namonge ni kati ya kata  17 za Wilaya ya Bukombe yenye vijiji vinane na vitongoji 36 ambayo imeendelea kupiga hatua ya maendeleo kwa kuwa na mtandao mrefu zaidi wa barabara kuliko kata zingine.

Dkt. Biteko amesema hayo Novemba 25, 2024 wakati akihutubia katika Kampeni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wilayani Bukombe zilizofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Namonge mkoani Geita.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000