TPF – NET MAKAO MAKUU YA POLISI YAWAKUMBUKA WATOTO NJITI 06 MACHI 2024 DODOMA 

Katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto la Jeshi la Polisi Nchini ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Mtandao wa Polisi Wanawake Tanzania (TPF – Net) Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Maria Nzuki March 06, 2024 amewaongoza Mtandao wa Polisi Wanawake (TPF – Net) Makao Makuu ya Polisi Dodoma katika kutoa msaada kwa watoto njiti na watoto wenye uhitaji maalum katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa  Dodoma. 

Akikabidhi msaada huo wa vitu  vyenye thamani ya Tsh 1,495,000,  DCP Nzuki alisema kuwa Mtandao wa Polisi Wanawake Makao Makuu ya Polisi wameona umuhimu wa kupeleka zawadi kwa Watoto wenye uhitaji maalum na Watoto njiti ikiwa ni kuunga mkono jitihada za Mheshimiwa  Rais Samia Suluhu Hassan ya kusogeza huduma bora kwa wananchi hasa katika maeneo ambayo huduma hiyo haipo.  

 Aidha, amewataka wananchi ambao kwa sasa ni wazima kiafya kushirikiana ili kuhakikisha kuwa wagonjwa ambao wapo hospitali wanapata mahitaji yanayohitajika ili afya zao ziweze kuimarika.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000