Tanzania iko imara kiuchumi- Fitch

Tanzania yawekwa kwenye viwango vya B+ na Fitch kwenye masuala ya uchumi na ikitanguliwa na viwango vya B vilivyowekwa na Moodys hapo awali.

Tanzania inakuwa ni nchi pekee kwenye ukanda wa Africa Mashariki na imewekwa kwenye kundi B2 ikizipita Kenya, Uganda , Rwanda ambazo zina kiwago hasi(negative)

Kwenye ripoti hiyo ya karibuni nchi ambayo iko na Tanzania kwenye kundi moja ni Jordan, hii ikiwa na maana kuwa uchumi wa Tanzania sasa na aiku zijazo ni stahimilivu sana.

Viwango vya Fitch na Moodys ndivyo vinavyotumika kupima uwezo na ukakamavu wa uchumi wa nchi husika na uwezo wake wa kukopesheka.

Kwa matokeo haya ni wazi kuwa serikali ya Rais Samia inasimamia uchumi vyema na vigezo vyote vinavyotumika kupima uchumi(macro indicators) vinaashiria ukuaji huo.

Wizara ya fedha na waziri wake inahitaji pongezi kubwa sana kwa matokeo haya kwa sababu inaonekana jinsi ilivyo imara kwenye kusimamia sera za fedha na mipango ya uchumi wa Tanzania.

Kwa habari zaidi fuatilia link;

fitchratings.com/research/sover…

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000