TAMISEMI YAWAJENGEA UWEZO WASIMAMIZI WA MPANGO WA KUSAIDIA MAKUNDI NA MAKABILA YALIYOHATARINI KUTOWEKA

Morogoro

OFISI ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), imefanya kikao kazi cha kuwajengea uwezo wasimamizi na watekelezaji wa mpango wa kuwasaidia watu wa makundi maalum na makabila ya asili yaliyo katika hatari ya kutoweka (Vulnerable group).

Kikao kazi hicho kimefanyika leo Januari 29, 2025  katika Chuo cha Ualimu Kigurunyembe Mkoani Morogoro na kimehusisha Waratibu wa mpango wa shule salama, Maofisa Maendeleo ya Jamii na Maofisa Ustawi wa Jamii wa ngazi ya Mkoa na Halmashauri.

Mratibu wa Shule Salama, Ofisi ya Rais – TAMISEMI Hilda Mgomapayo ameeleza kuwa kikao hicho ni cha kutathmini hali ya utekelezaji kufuatia ziara iliyofanyika ya  kuwatembelea makundi maalum  na makabila ya watu wa asili kwenye mikoa ya Dodoma, Singida, Manyara, Arusha na Simiyu.

Amesema pamoja na ziara hiyo Maofisa hao walijengewa uwezo  jinsi ya  kuandaa mpango mkakati wa kusaidia makundi maalumu  na makabila ya asili.

Mratibu huyo ametoa wito kwa wataalamu hao kushughulikia  na kufuatilia  kwa haraka changamoto na malalamiko kuhusiana na makundi maalumu yanapojitokeza.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000