Rais Samia atoa ombi kwa Yanga juu ya sakata la Fei Toto

Rais Samia ameitaka klabu ya Yanga kumalizana na mchezaji wao Fei Toto aliyevunja mkataba wa kuendelea kubakia klabuni hapo.

Kauli hii imetokewa leo wakati Mheshimiwa Rais akiongea na wachezaji wa Yanga na wageni waalikwa kwenye halfa iliyofanyika Ikulu kuwapongeza Yanga kwa kucheza fainali za kombe la shirikisho na kuukosa ubingwa baada ya USMA ya Algeria kushinda kwa goli la ugenini mwishoni mwa wiki iliyopita.

Hatua hiyo ya Rais imekuja masaa machache baada ya rais wa Yanga Injinia Hersi kunukuliwa leo kwenye mahojiano yake na chombo kimoja cha habari kuwa suala la Fei Toto yeye atasimamia sheria na alikwenda mbali zaidi na kusema Fei Toto hawezi kupewa medali kwa kuwa ni dogo jeuri.

Baada ya ombi hilo la Mheshimiwa Rais kwa uongozi wa Yanga , sasa wadau wanatega masikio kusikia kama klabu ya Yanga wataufyata mkia na kufuata matakwa ya Fei Toto kuondoka klabuni hapo au watasimamia sheria kama alivyojinasibu Injinia Hersi leo asubuhi.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000