RAIS MWINYI:TUSIMAMIE MALEZI NA MAADILI YA VIJANA NA WATOTO.

Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt, Hussein Ali Mwinyi  amezitaka familia  kuweka dhamira ya Kusimamia  Malezi ya Vijana na Watoto ili kuwa  na Taifa lenye Heshima na Maadili. 

Rais Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika Sala ya Ijumaa Masjid Al Sahar Kwarara, Njia nne, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 2 Mei 2025.

Aidha Rais Dkt, Mwinyi amesema mambo mengi yanayojiri hivi  sasa  ndani ya Jamii yakiwemo ya Wizi na Uharibifu wa Miundonbinu ya Serikali  yanafanywa na Vijana waliokosa Malezi Bora na Maadili ya Dini .

Amefahamisha kuwa Mustakabali wa Nchi yoyote Unahitaji Malezi ya Vijana na Watoto waliolelewa kwa Maadili Ili kuwa Watu wema na Wazalendo wa Nchi Yao.

Ameeleza kuwa ni lazima  kila Mmoja kuwa na dhamira ya  Kusimamia Malezi ya Vijana ndani ya familia ili kuwa na Watu wema watakaokuwa Viongozi wa baadae.

Halikadhalika Rais Dkt, Mwinyi amewakumbusha Waumini hao Umuhimu wa Kuendelea kuiombea Nchi Amani hasa wakati Huu ikielekea katika Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba Mwaka Huu.

Kwa upande mwingine Rais Dkt.Mwinyi amesisitiza kuwa bado Serikali inakusudia kutekeleza mambo mengi zaidi ya Maendeleo  katika Nyanja tofauti hivyo Suala la kuwepo kwa Amani ndio Kipaumbele Muhimu zaidi

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000