RAIS MWINYI : SMZ IMEWEKA MKAZO KUIFUNGUA PEMBA KIUCHUMI 

Zanzibar,

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali imeweka mkazo maalum wa kuifungua Pemba kiuchumi kwa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege,Bandari na miundombinu ya Barabara.

Dk. Mwinyi alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na Ujumbe Maalumu wa Serikali ya Uingereza ulioongozwa na Mhe.Kate Osamor [MB],Mjumbe maalumu wa Biashara wa Serikali ya Uingereza kwa Afrika Mashariki.

Katika mazungumzo hayo Alisema, suala la Ujenzi wa Miundombinu ya Barabara umefikia asilimia 70% sambamba na maendeleo ya ujenzi wa uwanja mpya wa Ndege wa Pemba pamoja na Bandari.

Ameufahamisha ujumbe huo kuwa kuchelewa kufunguka kiuchumi kwa kisiwa cha Pemba,kunatokana na ukosefu wa miundombinu hio mbayo ndiyo chachu ya maendeleo ya ukuaji wa uchumi katika taifa lolote duniani. 

Akizungumzia Kilimo cha Mwani ambacho kina mwamko mkubwa kwa wanawake wa Zanzibar,Rais Dk.Mwinyi kwa Zanzibar ameeleza kuwa licha ya ongezeko la uzalishaji wa zao hilo, bado bei ya zao hilo hairidhishi kulingana na kile kinachozalishwa na kuutaka ujumbe huo kuangalia namna bora ya kuwakwamua wazalishaji wa mwani kwa kuliongezea thamani zao hilo.

Rais Dk.Mwinyi ametoa Rai kwa Ujumbe huo kwamba Zanzibar bado inahitaji wawekezaji zaidi wa Sekta binafsi ili kufikia Dira ya  Maendeleo ya Zanzibar kiuchumi ya 2050.

Naye Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Balozi Marianne Yang ameeleza kuridhishwa kwa kasi ya maendeleo  inayofikiwa na Zanzibar katika sekta zote za kuimarisha uchumi na kuahidi ushirikiano kati ya pande mbili hizo.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000