RAIS MWINYI AWASILI JIJINI DODOMA

Dodoma

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, ambapo amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule, pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama wa mkoa huo leo, tarehe 27 Juni 2025.

Rais Dkt. Mwinyi atashiriki katika mkutano wa kulifunga Bunge la 12, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, atalihutubia Bunge hilo, Bungeni, Dodoma.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000