RAIS MWINYI AWASILI DODOMA.
Published on: 2 days ago
Dodoma
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mama Mariam Mwinyi ameondoka Zanzibar na Kuwasili Jijini Dodoma kwa ajili ya shughuli za kikazi.
Katika Uwanja wa ndege wa Dodoma , Rais Dk.Mwinyi amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule na viongozi mbalimbali wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi na Vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Aidha, Rais Dk.Mwinyi akiwa Dodoma atashiriki vikao vya kikatiba vya Chama Cha Mapinduzi ngazi ya Taifa vikiwemo Halmashauri Kuu ya CCM Taifa , Kamati Kuu ya CCM Taifa na Mkutano Mkuu Maalum wa CCM utakaofanyika tarehe 18 na 19 Januari 2025 Jijini Dodoma.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000