RAIS MWINYI AKUTANA NA TUME YA MABORESHO YA KODI
IKULU,Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, amekutana na Tume ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Maboresho ya Kodi, Ikulu Zanzibar iliyofika kujitambulisha.
Katika mazungumzo na Tume hiyo iliyoongozwa na Mwenyekiti wake, Balozi Ombeni Sefue na ujumbe wake, Rais Dk. Mwinyi wamejadili mambo mbalimbali ikiwemo mapendekezo yatakayozishauri Serikali mbili za SMZ na SMT kuhusu masuala ya kodi.
Aidha, Rais Dk. Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuteua Tume hiyo na kueleza kuwa itasaidia kuimarisha na kubadilisha mifumo ya kodi kwa Serikali zote mbili za SMZ na SMT.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000