RAIS MWINYI AELEKEA UINGEREZA KUSHIRIKI MKUTANO WA CTIS

Dar es Salaam

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe, Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameondoka nchini leo na kuelekea Jijini London, nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi kuanzia tarehe 6 hadi 9 Aprili 2025 kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano wa Biashara na Uwekezaji wa Jumuiya ya Madola (Commonwealth Trade & Investment Summit 2025).

Katika ziara hiyo Rais Dkt.Mwinyi matukio mengine atakayoshiriki ni kukutana na Viongozi waandamizi wa Serikali ya Uingereza na Taasisi zake, atakutana na  Diaspora wa Tanzania waliopo nchini Uingereza, atakutana na Sir Tony Blair , Waziri Mkuu Mstaafu na Kiongozi wa Tony Blair Institute (TBI), pia atakutana na wadau wa uwekezaji katika uchumi wa bluu.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi atakutana na wadau wa  uwekezaji katika sekta ya utalii, filamu, viwanda, nishati ikiwemo pia mafuta na gesi.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi atashuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano baina ya Wizara ya Uchumi wa Buluu na Chuo Kikuu cha Kent kwa ajili ya utafiti wa kilimo cha Mwani pamoja na MOU kati ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Kampuni ya Perry Engineering ya Uingereza kuhusu usambazaji wa mbegu za mwani.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000