NIMEMPOTEZA RAFIKI NA KAKA MLEZI : NCHIMBI AKIMZUNGUMZIA HAYATI LOWASSA

Taarifa ya kifo cha Edward Ngoyai Lowasa kwangu ilikuwa habari mbaya sana.

Nimepoteza rafiki, kaka na mlezi, Chama Cha Mapinduzi na Tanzania tumempoteza mtu. Ni pigo kubwa sana kwa Nchi yetu.

Lowasa alikuwa MwanawaAfrika, Mtu wa Maamuzi Magumu na alikuwa mchapakazi haswa na hili sote tunakubaliana nalo.

Dkt. Nchimbi amesisitiza kwamba funzo kubwa tuliloachiwa na Hayati Lowassa ni kuwa, uongozi ni utumishi kwa watu; hivyo, ni lazima viongozi wawatumikie watu wote bila ubaguzi na wawaonyeshe upendo wa dhati.

PICHA YA PILI I Katibu Mkuu wa CCM Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi akibadilishana mawazo na kusalimiana na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali katika shughuli ya kuuaga mwili wa aliyekuwa Waziri Mkuu Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Komredi Edward Ngoyai Lowasa Kijiji cha Ngarash Wilayani Monduli Mkoani Arusha.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000