NIGERIA NA IVORY COAST ZATINGA FAINALI ZA AFCON

Hatimae Mabingwa mara tatu wa michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Nigeria wamefanikiwa kuingia kwenye fainali za AFCON baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Afrika Kusini.

Ivory Coast, wenyeji wa michuano hiyo ilifanikiwa kutinga fainali baada ya kuiondoa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Nigeria ilipata ushindi huo baada ya mlinda lango Stanley Nwabali, kuokoa mikwaju miwili ya penati. Timu hizo zilimaliza mchezo kwa sare ya 1-1 jana Jumatano.

Nigeria ilishindwa mara tano kati ya mara sita katika hatua ya nusu fainali za michuano hiyo huko nyuma na sasa itakabiliana na wenyeji Ivory Coast katika fainali hizo zitakazochezwa siku ya Jumapili.

William Troost-Ekong aliipatia Nigeria bao la kuongoza, kabla ya Afrika Kusini kujipatia bao la kusawazisha katika dakika za mwisho, lililofungwa na Teboho Mokoena.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000