MBUNGE UMMY MWALIMU ASHIRIKI MKUTANO WA HADHARA WA MKOA TANGA KUUNGA MKONO MAAMUZI YA MKUTANO MKUU CCM TAIFA KUMPITISHA DKT SAMIA KUWA MGOMBEA URAIS 2025
* Amesema kwa mambo makubwa ya maendeleo yaliyotekelezwa Tanga Mjini wanaunga Mkono Maamuzi ya Mkutano Mkuu kwa asilimia 100 na watampa Dkt Samia kura za kishindo Octoba 2025
* makundi ya wananchi wakiwemo Wavuvi, Mafundi Gereji, madereva, Wajane, Bodaboda, Wahudumu wa Afya nao wajitokeza kwa wingi kuunga mkono Dkt Samia kupitishwa kugombea.
—-
Mbunge wa Jimbo la Tanga Mhe Ummy Mwalimu tarehe 28/1/2025 ameshiriki mkutano wa hadhara uliondaliwa na CCM mkoa wa Tanga chini ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Kamati Kuu Ndugu Rajab Abdulrahaman uliofanyika katika viwanja vya Community Center Kata ya Makorora Jijini Tanga. Mkutano huo umefanyika kwa malengo makuu mawili, moja, kuzindua Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa CCM na pili Kuunga Mkono Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa ya Kumpitisha Dr Samia Suluhu Hassan kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muunguno wa Tanzania mwaka 2025, Dr Husein Ally Mwinyi kuwa mgombea Urais wa Zanzibar 2025 na Ndugu Emmanuel Nchimbi kuwa Mgombea Mwenza 2025.
Akiongea katika mkutano huo Mhe Ummy alieleza kuwa akiwa ni mbunge wa kuchaguliwa na wananchi wa Tanga Mjini anayo mamlaka ya kuwakilisha maoni yao kuwa watu wa Tanga Mjini wanaunga mkono kwa asilimia 100 Maamuzi ya Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa kumpitisha Dkt Samia kuwa kuwa Mgombea Urais katika Uchaguzi Mkuu ujao wa 2025.
Mbunge Ummy alieleza kuwa sababu za wananchi wa Tanga Mjini kuuunga mkono uamuzi huu ni kutokana na kazi kubwa na nzuri za maendeleo zilizofanywa na Rais Samia katika Jimbo la Tanga Mjini katika minne na nusu ya uongozi wake. Kazi za Dkt Samia Tanga Mjni zinaonekama katika Sekta za Elimu, Afya, maji, Umeme hasa maeneo ya vijijini, uboreshaji wa miundombinu ya barabara, mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kubwa zaidi ni Maboresho ya Bandari ya Tanga kwa kuongezwa kina na sasa meli kubwa zinatia nanga katika Bandari ya Tanga na hivyo kuleta fursa za kiuchumi, biashara na uwekezaji Tanga. Mhe Ummy amesema kwa hili la Maboresho ya Bandari ya Tanga tu; Rais Dkt Samia hana deni na wana Tanga Mjini.
Mhe Ummy alimuhakikishia Mwenyekiti wa CCM Mkoa na wananchi kuwa Viongozi na wanachama wa CCM Wilaya ya Tanga watafanya kampeni usiku na mchana, za nyumba kwa nyumba ili kuhakikisha Dkt Samia anapata kura za kumwaga ili aendelee kuwa Rais wetu kwa miaka mingine mitano.
Hata hivyo Mhe Ummy amewataka wakazi wa Tanga Mjini kujitokeza kushiriki kwenye zoezi la maboresho la daftari la kudumu la wapiga kura wakati zoezi hilo litakapoanza mwezi Februari 2025 ili waweze kuandikishwa na kuweza kumpigia kura Dkt Sania, Mbunge na Madiwani watakaosimamishwa na CCM.
Mkutano huo wa hadhara ulihudhuriwa na wajumbe wa kamati ya siasa mkoa wakiongozwa na Mwenyekit wa CCM Mkoa na Mjumbe wa Kamati Kuu Ustadh Rajabu Abdurahmani, Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Balozi Dkt Matilda Burian, Wajumbe wa Kamati za Siasa za Wilaya za Mkoa wa Tanga wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tanga Meja Hamisi Bakari Mkoba, Viongozi wa Chama na serikali kutoka Wilaya mbalimbali za Mkoa wa Tanga sambamba na makundi ya wananchi wakiwemo Wavuvi, Mafundi Gereji, madereva, Wajane, Bodaboda, Wahudumu wa Afya.
Imetolewa na ;
Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tanga Mjini
29/1/2025
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000