MBUNGE MAVUNDE KUWAPATIA MEZA NA VIFAA VYA KISASA MAMA LISHE WA STENDI KUU YA MABASI DODOMA

Atatua mgogoro wa wamachinga na Mama Lishe kuhamishwa

Ashauri wasiondolewe katika maeneo yao kwa sasa

Ampongeza Mkurugenzi Kayombo kwa utatuzi wa changamoto kwa haraka

Awaasa wafanyabiashara wadogo kufuata utaratibu

Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde ameahidi kuwaboreshea mazingira ya utoaji huduma Mama Lishe wa Stendi Kuu Dodoma kwa kuwapatia meza nadhifu na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ya Chakula.

Mh Mavunde ameyasema hayo leo wakati wa mkutano wa wafanyabiashara wadogo,Mama Lishe na uongozi wa Halmashauri ya  Jiji la Dodoma kwa lengo la kutatua changamoto ya uhamishwaji wa wafanyabiashara hao katika maeneo ya stendi kuu Jijini Dodoma.

“Madhumuni ya ujenzi wa stendi hii ni kutoa huduma ya usafirishaji na pia kuchochea uchumi wa wananchi wa Dodoma kupitia biashara mbalimbali.

Nishauri uongozi wa Jiji kuwapangia utaratibu mzuri wafanyabiashara hawa wafanye biashara hii kwa muda na baadaye watarejea katika maeneo rasmi baada ya mzunguko wa biashara kuimarika sokoni hapa.

Nitawasaidia Mama Lishe meza nadhifu na vifaa vya kisasa vya kutolea huduma ili msichafue mazingira hapa na mtoe huduma kwa kuzingatia kanuni za Afya na usafi wa Mazingira”Alisema Mavunde

Naye Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma *Ndg. John Lipesi Kayombo* amesema Jiji limekubali ushauri wa Mbunge kwa masharti ya wafanyabiashara hao kupangwa vizuri na kusimamia usafi wa mazingira yao.

Wakishukuru kwa pamoja, Wafanyabiashara wadogo na Mama Lishe wa Stendi Kuu Dodoma wameishukuru serikalinya awamu ya sita chini ya Mh Rais Dkt. Samia S. Hassan* kwa kuwajali na kuwasikiliza na kumpongeza Mbunge Mavunde kwa kusimamia na kuwajali.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000