MBUNGE MAVUNDE AKABIDHI MAGARI YA WAGONJWA HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amekabidhi magari mawili ya wagonjwa kwa uongozi wa Hospital ya Benjamin Mkapa yaliyotolewa na serikali ya India.
Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika viunga vya Hospital ya Benjamin Mkapa huku yakishuhudiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma *Mh. Rosemary Senyamule* na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa *Dkt. Alphonce Chandika*.
![](https://admin-k.kigogomedia.com/app/uploads/2024/02/GF6xGSBWkAASDgi.jpeg)
“Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Dodoma Mjini tunaishukuru sana serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mh Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa magari haya ya wagonjwa ambayo yatasaidia kuwahudumia wananchi wetu.
Tumeshuhudia maboresho makubwa sana katika sekta ya Afya jijini Dodoma ikiwemo ujenzi wa vituo vya Afya,Hospital ya Wilaya na upatikanaji wa magari ya wagonjwa kwa vituo vya pembezeni na hivyo kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.
![](https://admin-k.kigogomedia.com/app/uploads/2024/02/GF6xGSBXEAA2oNq.jpeg)
Nitajitahidi kwa nafasi yangu kuhakikisha tunaongeza gari lingine la wagonjwa kwa kuwa hospital hii inahudumia watu wengi zaidi ya hospital nyingi za hapa Dodoma hivyo ni muhimu kuboresha eneo hili”Alisema Mavunde
Akitoa maelezo ya awali Mkurugenzi Mtendaji wa Hospital ya Benjamin Mkapa *Dkt. Alphonce Chandika* amesema magari hayo yatasaidia sana katika kusafirisha wagonjwa wa rufaa kutoka Hospitalini hapo na hivyo kutumia fursa hiyo kuishukuru sana serikali kwa magari hayo ya kisasa na yenye vifaa muhimu vya matibabu ambayo yatarahisisha utoaji huduma kwa wagonjwa.
![](https://admin-k.kigogomedia.com/app/uploads/2024/02/GF6xFg5XIAE26Al.jpeg)
Naye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma *Mh. Rosemary Senyamule* amemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maboresho makubwa ya sekta ya Afya mkoani Dodoma na kuutaka uongozi wa Hospitali ya Benjamin Mkapa kuyatunza magari hayo na kuhakikisha yanafanya kazi iliyokusudiwa.
![](https://admin-k.kigogomedia.com/app/uploads/2024/02/GF6xGSEWYAAYaNN.jpeg)
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000