Maroli yenye shehena ya mahindi yazuiliwa mpakani Holili

Wafanyabiashara wa kitanzania wanaosafirisha mahindi kuingia nchini Kenya wameandamana muda huu kwenye mpaka wa Holili kufuatia kuzuiliwa kuingiza shehena za mahindi na Kenya.

Msururu wa maloli umekwama mpakani hapo kufuatia mamlaka za Kenya kuweka kigingi na kuzuia mamia ya maroli hayo kuingia nchini Kenya.

Ikumbukwe tatizo hili limekuwa linajirudia kila mara hasa kwa wafanyabiashara wa kitanzania kuingiza mahindi nchini Kenya.

Madereva hao wamelalamika jinsi ambavyo wanasumbuliwa bila sababu ya msingi mbali na kauli za mara kwa mara za viongozi wa nchi hizi mbili kusema ni ruhusa kwa biashara ya nafaka kufanyika baina ya nchi hizi mbili.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000