Klabu ya Simba yafuzu kwa tabu sana.

Klabu ya Simba pamoja na kufuzu kwenda hatua ya makundi kwa kuchechemea lazima tukiri kuwa ni timu dhaifu sana na bomu inatocheza mpira kwa kubahatisha.

Kwa kilichotokea leo ni kama Simba ni timu ya mitaani tu imekusanya wahuni na kuwaambia waache kunywa pombe kwa siku mbili hivi halafu waingie uwanjani kucheza mpira.

Kwa aina hii ya uchezaji ni ndoto kwa timu hii kuvuka hatua ya makundi na kwa vyovyote vile uwezo wao ni mdogo sana kwenye haya mashindano na wasipokuwa waaangalifu kwenye hatua ya makundi watakwenda kuoga MAKAPU ya magoli. Washabiki wa Simba ni vyema mkajiandaa kisaikolojia maana hapa hakuna timu na huo ndiyo ukweli.

Kocha huyu hana mbinu na sidhani kama ni aina ya kocha ambaye alistaili kufundisha timu iliyoko kwenye mashindano makubwa hivi na kwa kweli lazima tuseme SIMBA IMEFUZU KIBAHATI NA ILIKUWA TIA MAJI TIA MAJI VIBAYA SANA LEO.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000