KIKUNDI CHA CHADEMA CHAANDAMANA
Kwa majigambo na kelele za kikundi cha CHADEMA na kujionyesha kwamba ni wakubwa kisiasa na ni kikundi kikubwa ni aibu na mshangao kwa kinachotokea! Chama kinachojiita kikubwa cha upinzani japo hakina wabunge wa kuchaguliwa ndani ya bunge wanashindwaje kuisimamisha Dar Es Salaam kwa maandamano?
Yaani wanakosa watu hata elfu 10 tu kukusanyika pamoja na kuandamana? Na uchache huo ni Dar Es Salaam yaliko makao makuu ya kikundi chao, hivi wakienda sehemu kama Lindi au Tabora wataandamana na nani? Hii imetosha kuwaonyesha kuwa kelele za mitandaoni siyo uhalisia huko kwa wananchi na haya ndiyo yanawakuta kila siku mnapokuwa mnafikiri siasa mnazozinafanywa mitandaoni zina uhalisia kwa wananchi.

Ripoti wetu amehangaika sana kumtafuta Lissu Antipas au mke wake au wale watoto wake walioko Marekani kuona kama wamekuja kwenye maandamano lakini hakumuona mkewe wala watoto wake akina Edward! Amehangaika sana kumtafuta Maria Sarungi lakini hajamuona yeye au mume wake au baba yake wakiwa kwenye maandamano hayo.
Sasa tunajiuliza watu hawa wakikuwa wanahamasisha maandamano halafu wao hawana hamu ya kuandamana au? Kwa kifupi CHADEMA hawana huo ukubwa wanaopayuka kuwa wanao na kelele kuwa wao ni chama chenye nguvu na watu. Hawana huo ukubwa na hawana hao watu zaidi ya kelele za mitandaoni!
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000