KATIBU MKUU WIZARA YA AFYA AZUNGUMZA NA MKURUGENZI MSAIDIZI SHIRIKA LA AFYA DUNIANI ANAESHUHULIKIA TAKWIMU.

Katibu Mkuu Wizara ya Afya Dkt. John Jingu akutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu Msaidizi wa Shirika la Afya Duniani anayeshughulikia takwimu na uchambuzi Dkt. Samira Asma.

Katika mazungumzo yao wamekubaliana kuanzisha ushirikiano wa kuiwezesha Tanzania kuongeza kasi ya utekelezaji wa viashiria vya kipaumbele vya nchi katika kufikia malengo endelevu.

Timu kutoka makao makuu ya Shirika la Afya duniani itaungana na timu ya kanda ya Afrika na kushirikiana na wataalam wa wizara ya afya katika uchambuzi wa takwimu na uanzishwaji wa miradi mahsusi ya kuongeza kasi ya utekelezaji katika kufikia viashiria hivyo.

Katika mkutano huo, Mkurugenzi Mkuu Msaidizi Dkt. Asma ameipongeza Tanzania kwa kupiga hatua kubwa za kupunguza vifo vya mama na mtoto ambapo matokeo ya Utafiti wa “Demographic Health Surveys ” ya mwaka 2022 yalionyesha kupungua kwa vifo kwa asilimia 80 ikiwa imechangiwa na uwekezaji mkubwa wa serikali ya awamu ya sita katika afya za msingi.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000