Kaizer Chiefs watembelea Ikulu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dokta Hussein Mwinyi ameushukuru uongozi wa klabu ya Yanga kwa kuileta timu ya mpira wa miguu ya Kaizer Chiefs kutoka Afrika Kusini kuja kutalii Zanzibar baada ya kushiriki kwenye tamasha la klabu ya Yanga maarufu kama siku ya wananchi lililofanyika mwishoni mwa wiki jijini Dar Es Salaam.
Ameyasema hayo alipokutana na na timu ya Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini waliofika Ikulu Zanzibar wakiwamo viongozi na wachezaji wakiambatana na viongozi wa klabu ya Yanga. Aidha, Rais Dokta Mwinyi amesema Zanzibar ni nchi ya utalii ikiwemo utalii wa fukwe za bahari na mji mkongwe huko Zanzibar.
Rais Dk.Mwinyi alisisitiza kuwa kufika kwa Kaizer Chiefs kutembelea Zanzibar ni fursa muhimu ya kuitangaza Zanzibar huko Afrika ya Kusini na kimataifa kupitia utalii wa michezo ambayo ni ndoto yake ya muda mrefu.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000