GWAJIMA ALIKUWA ANAPIMA KINA CHA MAJI KWA MIGUU

(na mchambuzi wetu) 

Ni Jumapili leo na lilojiita kanisa la ufufuo la bwana Gwajima limepigwa kufuli na zile kelele zake zote zimeyeyuka kama barafu! Na bwana Gwajima yuko mafichoni anakimbia kutiwa nguvuni na polisi!. 

Huyu mtu alisema hakuna mtu wa kulifunga kanisa lake!. Lakini tunamkumbusha kuwa leo ni Jumapili vipi kuna misa inaendelea? Tunakusanya sadaka leo au? Mbona haonekani? Au atasalisha online au kwa bluetooth? 

Kinachomkuta kwa sasa  Gwajima ni matokeo ya kutaka kupima kina cha maji kwa miguu badala ya kutumia fimbo sasa matokeo yake amezama na amekwenda na maji!..

Hakuna dola au serikali inayoweza kuruhusu mtu toxic kama Gwajima akatumia jukwaa la analoliita ni kanisa lake kutaka kuleta vurugu na chuki miongoni mwa watanzania!. Yaani Gwajima alijiona kwa kuwa yeye ni Sukuma Gang na wadanganyana kwenye vikao vyao kuwa wanaweza kuitikisa serikali basi anaweza kutamka lolote analolitaka!.

Gwajima ni Mbunge! Alishindwa nini kuyaongea haya akiwa Mbunge huko bungeni ili kauli zake zilindwe na kanuni za bunge? Kuacha kufanya hivyo kulikuwa na maana kuwa alichotaka kufanya ni zaidi ya alichofanya na kimetafsiriwa kuwa alitaka kuleta uchonganishi kati ya serikali na watu wake!..

Sasa unapofikia hatua hiyo maana yake umeamua kuchokozana na dola na serikali na inapokunjua makucha yake ndiyo hivi sasa kanisa limefungwa na huna cha kufanya!. Kwa huyo hatutaki kusikia milio hapa isiyo na maana kwa kuwa Gwajima huyu hakuwahi jupanua mdomo wake kuongelea matukio kama haya wakati wa uongozi wa swahiba wake Kambale!.. kwa hiyo asijione ni mwema sana kwa watanzania kwa kuongea mamno haya sasa na akajiona anawatetea watu ! Gwajima ni jitu la maslahi na fursa na si vinginevyo!..

Kitendo cha Gwajima kusema hakuna mwenye uwezo wa kulifungia kanisa lake kilikuwa na maana ya kudharau kwa wazi kabisa mamlaka za serikali  na kujiona kuwa hakuna mtu anaweza kumfanya kitu au kumgusa! Haya swali nauliza ni Je? Leo kuna watu pale kabisani kwake wanaasali muda huu? Vipi mbona yeye mwenyewe kakimbia na kujificha kusikojulikana mpaka bungeni kashindwa kuhudhuria vikao? Kwani anaogopa nini?  

Sasa alipokuwa anasema hakuna wa kumfanya kitu haya yanayoendelea ndiyo kufanywa vitu kwenyewe ambako alikuwa hajui kunafananaje? Halafu nyie TANESCO hivi lile kanisa si lipo kwenye eneo la hifadhi ya zike nyaya za umeme? Au siku hizi mnaruhusu watu kujenga maeneo ya hifadhi ya barabara na umeme? 

Sasa hili liwe fundisho kwa watu wanaofuata mikumbi tu ya hawa watu! Kama yeye kajificha na anaogopa kujitokeza na kuzitetea kauli zake je? Nyie anaohazwa ujinga kuwa muandamane aijui muitete hii nchi mna hali gani?

Nilitegemea kwa mikwara ile ya Gwajima leo angekuwa kanisani muda huu anakusanya sadaka lakini haonekani yaani! 

MWISHO ni kuwa Sukuma Gang wanajidanganya sana na hawataki kukubali kabisa kuwa zama zao zilikwishafika mwisho na linapokuja suala la uongozi na hasa urais wa nchi hii ni Mungu anayeamua na wao kama Sukuma Gang hawana haki ya kujimilikisha hii nchi!..Kwa hiyo waendelee na vikao vyao vya kujazana ujinga halafu tuone mwisho wao utakuwa nini!..

#KigogoMediaUpdates

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000