GHARAMA KUBWA UZALISHAJI GESI ASILIA NDIO SABABU YA UBIA SERIKALI SEKTA, BINAFSI
GHARAMA kubwa ya uzalishaji gesi asilia imetajwa kuwa sababu ya serikali kuingia ubia na sekta binafsi ili kuzalisha rasilimali hiyo muhimu.
Akizungumza leo Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema sekta binafsi itato mitaji, ujuzi, ubobezi na teknolojia ya kisasa katika uzalishaji wa gesi hiyo.
“Kwa wastani umeme unaozalishwa kwa kutumia gesi asilia ni takribani asilimia 65 mpaka 70 ya umeme wote unaozalisgwa nchini,” ameeleza Rais Samia.

Amesema kwamba tatizo la umeme nchini lingekuwa kubwa zaidi kama Tanzania isingekuwa na gesi asilia.
“Kwa sekta hii ya gesi ni lazima wananchi wa Lindi na Mtwara waanze kuona manufaa ya uwepo wa kampuni kubwa, ni matumaini yangu kwamba ajira zile ambazo hazitakuwa za kitaalamu sana zitakwenda kwa wananchi waliozunguka eneo hilo,” amedokeza Rais Samia.
Rais Samia ameshuhudia utiaji saini mikataba ya mauziano ya hisa na uendeshaji wa kitalu cha Mnazi Bay baina ya TPDC na Kampuni ya Maurel & Prom.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000