DP World yapewa bandari ya Dar Es Salaam

Bunge la Tanzania linajadili azimio la kuitaka serikali kuingia makubaliano ya uendeshaji na uboreshaji wa bandari ya Dar Es Salaam.

Kwa maumivu na utapeli uliofanywa na TICTS na akina Karamagi kwa miaka yote hiyo , uamuzi huu ulikuwa ni wa lazima na sasa ni jukumu la bunge kuona wapi wanaweza kuboresha na wapi kupunguza lakini ni hatua nzuri kusonga mbele.

Hilo la miaka 100 ni jambo la kuzungumzika na haliwezi kuwa kikwazo cha mambo haya kufanyika na mkataba wa uendeshaji wa bandari hii kufanyika.

Sasa hapa ndipo tunapolitaka bunge letu kuwa makini na kupitia kwa umakini sana kila kipengele na kuamua na kuushauri serikali kwa busara

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000