DC SAKINA AKABIDHI MKOPO WA MILIONI 500 MBOGWE

Mbogwe 

MKUU wa Wilaya ya Mbogwe Mheshimiwa Sakina Jumanne  amekabidhi hundi ya Shilingi Milioni 500 kwa Wanawake, Vijana na Makundi Maalum.

Fedha hizo  ni sehemu ya Shilingi Milioni 800 zilizotengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe kutolewa kama mkopo wa Asilimia 10 ya Mapato ya ndani.

Akizungumza leo  Januari 16, 2025 

Sakina amesema makundi yaliyopewa mikopo ni pamoja na kundi la vijana ambapo kwa namna ya tofauti vijana wamekabidhiwa pikipiki 20 ili wafanye shughuli za ujasiriamali na kujiletea maendeleo.

Aidha, Sakina amewataka wananchi wa Mbogwe kutambua kazi kubwa inayofanywa na Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kuwaletea wananchi maendeleo ambapo katika mwaka wa fedha 2024/2024 Mbogwe imetenga jumla ya Milioni 800 kwenda kwa wananchi kujiletea maendeleo.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya  amewataka watumishi wa  Halmashauri ya Mbogwe hususan Idara ya Maendeleo ya Jamii  kuelimisha  wananchi kujiunga kwenye vikundi ili wanufaike na fedha zilizotengwa kutolewa kwa wananchi kama mkopo kwani kama hawatawaelimisha wananchi na kuwasaidia kujisajili kwenye mfumo, fedha nyingi zitakosa wakopaji wenye sifa.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000