BoT kuna nini?

Kwa wiki ya pili sasa benki kuu ya Tanzania imeshindwa kuidhinisha malipo mbalimbali ya idara za serikali na wafanyakazi wa serikali sababu ikielezwa kuwa kuna changamoto ya mtandao.

Ikumbukwe kuwa idara zote za serikali zinapitisha malipo yao benki kuu kabla ya kuruhusu fedha kwenye kwenye mabenki ya biashara ambako idara za serikali zina akaunti.

Wiki mbili nzima watu wameshindwa kusafiri na kufanya kazi na benki kuu imekaa kimya bila kutoa tamko la maana kuhusu ucheleweshwaji huu.

Watanzania wana haki ya kujua kwa nini zaidi ya wiki mbili benki kuu haifanyi malipo? Tatizo gani kubwa kiasi hicho linalofanya wiki mbili msiidhinishe malipo? Kama benki kuu yetu inakumbwa na tatizo la kimtandao zaidi ya wili mbili basi tuna shida ya kiuongozi ndani ya benki kuu na shida ya kiteknolojia kwa sababu jambo hilo ni hatari sana. Tunawezaje kukaa wiki mbili shughuli za malipo ndani ya serikali zinasimama? Au hatuna hela? Tunasingizia mambo ya mtandao?

Uongozi wa benki kuu mnatakiwa kuwa wakweli na wawazi na kusema tatizo ni nini haswa kuliko kukaa kimya na kutoa sababu laini laini tu kuwa kuna shida ya mtandao.

Fikirieni nchi imesimama wili mbili malipo hayafanyiki kwenye idara na wafanyakazi wa serikali. Hiyo maana yake ni mbaya sana na inahitaji maelezo.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000