Basra Textile Mills ni Wahujumu uchumi na hatari kwa uchumi wa Tanzania

Wakati serikali kwa nia njema kabisa imeondoka VAT kwenye bajeti ya 2023 ,kwa bidhaa zote za nguo zinazotengenezwa kwa pamba ya Tanzania lakini kampuni ya BASRA TEXTILE MILLS LTD iliyoko Zanzibar inamilikiwa na wasomalia imekuwa inakwepa ushuru na kufanya ujanja ujanja kiasi kwamba sasa sekta ya nguo na kilimo cha pamba kinakwenda kufa.

Kampuni ya BASRA TEXTILE MILLS LTD iliyoko Zanzibar inanufaika na msamaha huu wakati hainunui pamba kwa wakulima na inachokifanya ni kuagiza vitambaa wanavyotumia kutengezeza nguo kutoka nje ya nchi na kinachofanyika ni kutengeneza nguo Zanzibar na wanaleta bidhaa zao Tanzania Bara na hawalipi ushuru kabisa. Swali la kujiuliza Basra Textile Mills Ltd wananunua pamba wapi? Wananunua pamba Zanzibar? Kama hawanunui pamba kwa wakulima wanakuwaje wanapewa msamaha wa kodi ambao hauwahusu kabisa? Na wanakuwaje hawalipi ushuru wanapoleta bidhaa zao Tanzania bara? TRA mpo na haya yanatokea machoni penu? Au kuna namna inafanywa na hawa wasomali kiasi kwamba mmefungwa macho na hamuoni?

Tunajua kuwa serikali ya Zanzibar imeisamehe kampuni ya BASRA TEXTILE MILLS LTS kulipa kodi zote. Yaani wanalipa ushuru SIFURI kwa maana hawalipi VAT na duty. Hawalipi kabisa hata senti moja.

Chanzo chetu ndani ya TRA na ZRB kimetujulisha kuwa kampuni ya BASRA TEXTILE MILLS LTD imekuwa ikidanganya sana kwa mamlaka za mapato juu ya idadi ndogo ya malighafi wanazoingiza kwa ajili ya kutengeneza nguo. BASRA TEXTILE MILLS LTD wamekuwa wanataja idadi ndogo au pungufu ya urefu wa vitambaa wanavyoingiza nchi kwa ajili ya kutengeneza nguo ili kukwepa ushuru.

Kigogo Media tumefanikiwa kupata takwimu na kuona nyaraka hizi za kutisha sana jinsi ambavyo Basra Textile Mills Ltd wanavyodanganya mamlaka. Kwanza wanaingiza nchi polyester na siyo cotton kama ambavyo msamaha wa kodi unataka na tunajua kuwa karibuni waliingiza kilo 594,100 za vitambaa vya polyester greige ambazo ni sawa na mita 1,230,000 na cha kuchekesha walilipa TZS 4,121,777/= wakati wenzao wa bara kwa uzito huo na urefu huo huo wanalipa jumla ya TZS 895,180,800/= . Katika hali hii hawa wanashindana vipi na viwanda na wafanyabiashara wa Tanzania Bara? TRA nini kazi yenu kulinda wafanyabiashara wa bara dhidi ya huu uhuni wa Basra Textile Mills Ltd?

Sasa swali ni kwa namna gani Basra Textile Mills Ltd wamaweza kushindanishwa na wazalishaji wa bara na kwa hali hii ni wazi wanauwa soko na kuhatarisha biashara Tanzania Bara na kuhatarisha wakulima wa pamba wa Tanzania bara.

Hawa wasomali wanafanya uhujumu uchumi na mamlaka za kiserikali wanatakiwa kufuatilia na kuchunguza jambo hili kwa sababu haiwezekani makampuni haya yanatumia ujanja ujanja na kuja kuvuruga kilimo na zao la pamba na kunufaika na misamaha ya kodi kinyume na nia njema ya serikali.

TAKUKURU mpo,POLISI mpo na TRA mpo .. Haya mambo ni ya kuyatazama kwa haraka sana kwa sababu msipokuwa makini kinachokwenda kufanywa na hawa wasomali ni;

  1. Kuuwa kabisa zao la pamba na wanunuzi na watengenezaji wa nguo walioko bara hawataona haja ya kuendelea kushindanishwa na makampuni ya hivi ambayo yanakwepa kodi na kuna kila dalili yanalindwa na wakubwa
  2. Wakulima wataanza kukosa watu wa kununua pamba yao kwa kuwa wanunuzi hawawezi kufanya biashara isiyo na ulinganifu na kushindana na akina Basra textiles Mills Ltda ambao nio wakwepa kodi
  3. Viwanda vya bara vitafungwa na maelfu ya watanzania watakosa ajiri na hili litakuwa ni tatizo kubwa sana kwa Tanzania Bara na mzigo huu utakuwa wa serikali ya bara

Hili suala ni la kufanyiwa kazi na hii kampuni ishughulikiwe na kuchunguzwa haraka sana kwa sababu wanachofanya ni kukweoa kodi na kuhujumu uchumi na kutumia ujanja ujanja kuharibu soko la nguo na pamba Tanzania na madhara yake ni k makubwa sana huko mbele na lazima washughulikiwe

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000