AWESO AINGIA NAMTUMBO USIKU, AKABIDHI MABOMBA MTUMBATIMAJI NA KUTOA SIKU 60 KAZI IKAMILIKE

Namtumbo

Waziri wa Maji Mhe.Jumaa Aweso ametinga usiku kijiji cha Mtumbatimaji wilayani Namtumbo ambapo amekabidhi Mabomba ya Mradi wa Maji Mgombasi wenye gharama ya Shilingi Bilioni 2.7 uliofikia asilimia 78 ya utekelezaji wake na utakapo kamilika unatarajia kuhudumia wananchi zaidi ya 8,414 kutoka katika vijiji 3 vya Mgombasi, Mtumbatimaji pamoja na Nangero.

Akizungumza na wananchi wa Mgombasi Waziri Aweso amemtaka Mhandisi wa Maji wa Wilaya  kuhakikisha ndani ya siku 60 mradi huo uwe umekamilika ili wananchi hao wanufaike na huduma ya Majisafi na salama.

Aidha Mhe. Aweso amemuelekeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Eng Mwajuma Waziri alete timu ya wataalam kutoka Wizara ya Maji ije ifanye tathmini ya haraka katika Mji wa Namtumbo ili kuboresha huduma ya upatikanaji wa majisafi.

Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000