WAZIRI SAADA MKUYA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA KWENYE MKUTANO WA IMF
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango-Zanzibar, Dkt. Saada Mkuya Salum, aameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa kwa niaba ya Waziri wa Fedha wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb).
Ni mkutano wa Mfumo wa Kifedha wa Kimataifa uitwao (Global Financial Architecture) wa Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF).
Katika mkuano huo ambacho kimejadili ni kuhusu maombi ya Marekebisho ya vipaumbele kwa IMF na kushauri namna ya kuboresha dhamana ya ustahimilivu na uendelevu wa Shirika hilo wakati wa Mikutano ya Mwaka ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) inayofanyika jijini Marrakech, nchini Morocco.
Kikao hicho kimehudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Dkt. Natu el-Maamry Mwamba.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000