WATUMISHI 11 WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI KIGOMA
Kufuatia ripoti ya tume iliyoundwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa baada ya kubainika kuwepo kwa mtandao wa wizi huko Kigoma ,hatimaye watumishi 11 wamefikishwa mahakamani kwa tuhuma za uhujumu uchumi.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga mkoani Tabora Athuman Msabila na wenzake 10 wamefikishwa katika mahakama ya wilaya ya Kigoma kujibu tuhuma za uhujumu uchumi wakiwa watumishi katika Manispaa ya Kigoma Ujiji.
Akisoma mashtaka 11 yanayowakabili watuhumiwa hao wakili mwandamizi wa serikali Anosisye Erasto amesema watuhumiwa hao wanashtakiwa kwa pamoja katika kesi ya uhujumu uchumi namba 03/2023 wakiwa wametenda makosa ya kula njama kwa nia ya kutenda kosa, kughushi nyaraka, matumizi mabaya ya madaraka, kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya shilingi za kitanzania milioni 463.
Wakili mwandamizi Anosisye amewataja watuhumiwa hao kuwa ni pamoja na aliyekuwa Mkurugenzi wa manispaa ya Kigoma Ujiji na baadae kuhamishiwa wilayani Igunga Athuman Msabila, Aidan Mponzi, Tumsifu Kachira na Ferdinand Filimbi,Salum Said, Mosses Zahuye, Joel Shirima, Jema Mbilinyi, Kombe Kabichi, Frank Nguvumali na Bayaga Ntamasambilo wote wakiwa ni watumishi wa kada mbalimbali katika Manispaa ya Kigoma Ujiji na Ofisi ya Rais (TAMISEMI).
Hatua hii ni ya kupongeza sana kwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa kuchukua hatua hizi kali sana kwa watumishi wa serikali ambao ni majizi na wanafifisha jitihada za Mheshimiwa Rais kuwaletea maendelea watanzania kwa matendo yao haya.
Hivi ndivyo tunakata kuona viongozi wa serikali wanachukua hatua dhidi ya mambo haya kwa vitendo na siyo blah blah na Mheshimiwa Waziri Mkuu amelifanya hili kwa vitendo na mawaziri na viongozi wengine muige maana kama ni mfano basi ni huu hapa mmeshapewa.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000