WARSHA YA UPANGAJI BAJETI UNAOZINGATIA USAWA WA KIJINSIA
Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El- maamry Mwamba, amefungua warsha ya upangaji Bajeti unaozingatia usawa wa kijinsia wakati wa Mkutano wa ngazi ya juu wa Usawa wa Kijinsia wa Kanda ya Afrika, unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, jijini Dar es Salaam.
Dkt. Natu amesema kuwa, Warsha hiyo ni jukwaa muhimu ambalo linasaidia kujifunza mengi na kutekeleza mikakati ambayo itahakikisha sera za fedha sio tu zinafaa bali pia zinachangia kuwawezesha wanajamii wote.
“Kwa pamoja, tunaweza kutumia uwezo wa maarifa shirikishi kubuni mifumo ya kibajeti inayoshughulikia changamoto mahususi zinazoyakabili makundi mbalimbali ya watu wetu” aliongeza Dkt. Mwamba.
Warsha hiyo imehudhuriwa na Mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimaitaifa (IMF – Afritac East), Bi. Xiangming LI, Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika Mashariki, Kusini na Magharibi – UN WOMEN, Dkt. Maxime Houinato, na Wataalam wa ngazi ya juu kutoka IMF, UN Women, Tanzania, Burundi, Burkina Faso, Jamhuri ya Kidemokrasia Kongo, Eritrea, Ethiopia, Guinea, Ivory coast, Nigeria, Senegal, Kenya, Liberia, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Somalia, Afrika Kusini, Rwanda, Sudan ya Kusini, Zambia, Zimbabwe na Uganda.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000