Visasi na roho mbaya ya Kikwete na Kinana inavyotaka kuipa Tanzania rais wa hovyo 2030

ROHO MBAYA,WIVU, CHUKI na KISASI walivyo navyo wazee hawa wawili(Kinana na Kikwete) vina kila dalili ya kwenda kutupa rais bomu tena kama walivyofanya mwaka 2015. Ni roho mbaya na chuki zao na visasi vyao kwa mgombea fulani ndani ya CCM mwaka 2015 ndivyo vilivyopeleka Magufuli akawa Rais bila kutarajiwa na moto wake wote waliuona na wakaiachia nchi ina makovu mpaka leo.Kundi hili hatari la watu hawa ndani ya CCM liko kazini kuona wanafanya yaleyale waliyoyafanya kwenye uchaguzi wa 2005.
Sababu ile ile waliyoitumia kutumbukiza nchi kwenye matatizo makubwa sana ya kiuongozi mwaka 2015 ndiyo hiyo hiyo wanataka kuitumia mwaka 2025 na ikishindikana basi 2030 mvua inyeshe au jua liwake wamedhamiria kuwa January Makamba lazima awe Rais. Na wanataka hivyo kwa sababu wanataka kumtumia kulipa visasi kwa watu ambao wanasema sasa hivi wanalindwa na hawashughulikiwi hata wanapowakosoa wao na kuwasema hasa huyu Kinana.
Swali la kujiuliza kwa nini wanalazimisha awe Rais? Kwani kuna nini nyuma ya haya yote? Jibu ni kuwa walishapanga kumfanya awe Rais 2025 na kama siyo maarifa makubwa yaliyotumika kumtoa aliyekuwa mkuu wa idara ya usalama ambaye alikuwa sehemu ya mpango huu hatari basi mpango wao waliokuwa wanasuka na kupanga naye ulikuwa unamfanya January Makamba Rais wa Tanzania 2025 ndiyo maana kuondolewa kwake sasa kumeacha hasira na chuki kubwa sana kwa wazee hawa wawili hasa Kinana ambaye ni makamu wa CCM lakini ni kama amesusa kufanya kazi za chama na yuko busy na mambo yake mengine tu kisa ni kuvurugwa kwa mpango wake huu na kisa kingine ni hasira aliyo nayo juu ya suala la bandari na DP World ambapo dili lake la kuleta wachina waje kuwa mbadala wa TICTS kufyekelewa mbali. Isitoshe suala la yeye kusemwa ndani ya mkutano wa CCM kuwa ni mpinzani wa uwekezaji wa DP World limemkasirisha sana mpaka leo na kinyongo alicho nacho ni kikubwa sana kiasi kwamba ameapa lazima atalipiza kisasi tu kama alivyofanya kwa Lowassa ambaye aliwahi kumtuhumu kwenye siasa zao huko Arusha miaka ya 80 kuwa yeye ni msomali na siyo mtanzania. Sasa hivi anajipanga na ameorodhesha list ya watu wa kushughulikiwa kwa staili ya Sabaya mara watakapokuja kuweka Rais wao 2030. NI VISASI VISASI, CHUKI NA ROHOO MBAYA TUPU.
Wazee hawa wana haki ya kufanya wanayoyafanya kwa kuwa ni uhuru wao kufanya hivyo lakini bahati mbaya sana wanawezaje kufikiria hata kumbadilisha dini January Makamba ili tu akidhi kigezo cha ukristo ili kuwa Rais 2030 kama itashindikana 2025? Yaani wazee hawa wamekuwa wa hovyo kiasi hiki kweli? Kwani kama mnataka kutushughulikia tunaowakosoa sasa na kufilisi watu mnaosema wanalelewa na serikali sasa hivi na wamewazidi kwenye madili yenu inahitaji lazima Rais awe mwizi na mla rushwa January Makamba kufanya hayo? Si Rais yoyote tu anaweza kufanya hayo kama watu mnaowaandama na kuandaa listi yenu ili washughulikiwe kama wametenda makosa au?
Haya mambo mliyafanya sana wakati wa kundi lenu la wanamtandao miaka ile na mnataka awamu hii mtumie mbinu zile zile kufanya uharamia wenu na kuwawekea watanzania Rais ambaye ni bomu na ana roho mbaya kama Magufuli? Kwa nini mnakuwa wagumu kujifunza ushenzi na uhalifu aliofanya Magufuli kwa sababu ya roho mbaya zenu za kutokumtaka Lowassa? Hivi mnaona watu wamesahau haya mliyowafanyia? Hivi mnadhani watanzania ni wajinga kiasi hicho kweli? Au mnadhani nyie ndiyo binadmau sana ndani ya Tanzania na mna haki ya kuwaamulia mambo yao hasa linapokuja suala la uongozi wa nchi? Haiwezekani nchi hii muiweke mateka kwa matendo yenu na tamaa zenu na visasi vyenu vya kisiasa na watu na mwisho wa siku mnakuja kuwapa mateso watanzania.
Yalikuwa ni makosa makubwa sana kumrudisha Kinana kwenye siasa za Tanzania kwa sababu ni mtu mwenye kuamini kwenye visasi na kulipiza mambo kwa wale anaowaona na wabaya wake kisiasa na hata kijamii ndiyo maana ameweza kuwa na January Makamba muda mrefu kuwinda watu wanaowakosoa na kutaka kuwauwa ndani ya mipaka ya Tanzania na nje ya mipaka ya Tanzania.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000