TAHADHARI ZA KIUSALAMA KUELEKEA MCHEZO WA SOKA KATI YA SIMBA NA YANGA
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linatambua kuwa Novemba 05, 2023
kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa Jijini Dar es Salaam kutakuwa na mchezo wa soka
mashindano ligi ya NBC baina timu ya Simba na Yanga zote za Jijini Dar es Salaam . Mchezo huo utaochezwa saa 11 jioni.
Jeshi la Polisi linatambua mchezo huo utakuwa na mvuto wa hali ya juu, hivyo kutakuwa na
mkusanyiko mkubwa wa mashabiki wa soka wa timu hizo katika kiwanja hicho kutokana
ushindani wa timu hizo.
Kwa kulitambua hilo Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya usalama limechukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo huo. Ukaguzi wa hali ya juu utafanywa katika milango ya kuingia na hairuhisiwa mtu yeyote kwenda uwanjani na silaha ya aina yoyote, isipokuwa baadhi ya vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo.
Asiyekuwa na tiketi hataruhusiwa kusogelea uwanja huo au maeneo ya milango ya kuingia.
Tahadhari zote za kiusalama zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na baadhi ya barabara chache
kufungwa ili kupunguza msongamano wa kuelekea na kutoka uwanjani siku hiyo.
Jeshi linashauri mashabiki wa soka wafike mapema ili kuepusha usumbufu wa kuingia uwanjani
kwani milango ya uwanja huo itafunguliwa kuanzia saa nne (4) asubuhi.
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam linawatahadharisha baadhi ya mashabiki wenye
tabia chafu zisizo za maadili kujiepushasha nazo kwani majukwaani watakuwepo makachero
ambao watakuwa wakifuatilia kwa karibu vitendo vyote vya hovyo na baada ya mchezo
watakaohusika na makosa hayo watakamatwa ili kukomesha tabia ambazo sio za kistarabu
kwenye viwanja vya soka.
Jeshi la Polisi linawatakia mashabiki wa soka na timu zao kila kheri.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000