RAIS MWINYI AMEELEKEA DOHA,QATAR
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, jana tarehe 08 Disemba, 2023 ameondoka Zanzibar kuelekea jijini Doha, Qatar kuhudhuria Kongamano la Uchumi la Doha.
Akiwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Rais Dk. Mwinyi akiwa na mkewe Mama Mariam Mwinyi na ujumbe alioambatana nao aliagwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdullah, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Idrissa Kitwana Mustafa Mawaziri, Mwanasheria Mkuu wa S.M.Z Dk.Mwinyi Talib Haji,Mstahiki Meya Mahmoud Mohammed Mussa pamoja na vikosi ya Ulinzi na Usalama vya SMZ na SMT.
Unataka kutuma habari? Submit on tuma kwetu kupitia info@kigogomedia.com au WhatsApp 07000000